Image
Image

Beckenbauer kuchunguzwa na FIFA kwa hongo ya kununua kombe la Dunia na Wenzie 6.

Aliyekuwa Nahodha na kisha kocha wa timu ya taifa ya Ujerumani iliyotwaa kombe la dunia Franz Beckenbauer ametajwa katika orodha ya watuhumiwa 6 wanaoshukiwa kutoa hongo kununua kombe la dunia la mwaka wa 2006 huko Ujerumani.
Kamati ya maadili ya FIFA imetoa orodha wa watu 6 waliongoza kampeini hiyo ya kutwaa uwenyeji wa kombe la dunia.
Shirikisho la soka la Ujerumani lilipasua mbarika lilipofichua ripoti ya upelelezi ambayo ilimpelekea Nahodha huyo wa zamani wa timu ya taifa ya Ujerumani kukiri kuwa alifanya makosa wakati wa kuwania zabuni ya wenyeji wa kombe hilo la dunia.
Mnamo mwezi Oktoba mwaka uliopita, Beckenbauer, 70, aliomba msamaha kwa hatua na kauli alizotoa wakati wa kuwania uwenyeji wa mashindano hayo.
Ujerumani wakati huo iliishinda Afrika Kusini kwa kura moja pekee.
Ujerumani ilipata kura 12 dhidi ya 11 za Afrika Kusini katika uchaguzi uliofanyika mwaka wa 2000.
Orodha kamili
Franz Beckenbauer
Wolfgang Niersbach
Helmut Sandrock
Theo Zwanziger
Horst Schmidt
Stefan Hans.
Jarida la upekuzi la Ujerumani, Der Spiegel mwaka uliopita liliripoti kuwa waandalizi wa kombe hilo walitenga Euro milioni 6.7 kununua uwenyeji wa mashindano hayo.
Beckenbauer, Zwanziger, Schmidt na Hans awanachunguzwa kwa makosa ya kutoa hongo ilikuwashawishi wajumbe waipigie Ujerumani kura pamoja na kutoa zabuni kadhaa kwa wajumbe fulani.
Kwa upande wao Niersbach na Sandrock wanachunguzwa kwa kosa la kushindwa kuripoti ukiukwaji wa kanuni na maadili ya FIFA.
Beckenbauer aliiongoza kikosi cha taifa cha West Germany wakati huo kutwaa kombe la dunia la mwaka wa 1974.
Aidha aliifunza timu hiyo miaka 16 baadaye ilipoibuka mabingwa wa dunia nchini Italia.

Amewahi pia kuifunza timu za Marseille na Bayern Munich, ambako anaihumia kama rais.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment