Image
Image

Marekani yawaonya raia wake walio Ulaya na wanaopanga kuzuru bara hilo.

Marekani imewaonya raia wake walio Ulaya na wanaopanga kuzuru bara hilo kuhusu uwezekano wa kutokea kwa mashambulio mengine ya kigaidi.
Tahadhari hiyo imetolewa baada ya mashambulio kuua watu 34 katika mji wa Brussels Jumanne.
Wizaya ya mashauri ya kigeni ya Marekani imesema makundi ya kigaidi huenda yakatekeleza mashambulio karibuni.
“Makundi ya kigaidi yanaendelea kupanga mashambulio ya kuteketelezwa karibuni kote Ulaya, yakilenga hafla za michezo, maeneo ya kitalii, migahawa na uchukuzi,” taarifa ya wizara hiyo ilisema.
Raia wa Marekani wanaozuru Ulaya wametakiwa kuwa macho zaidi maeneo yenye watu wengi au wanapotumia mifumo ya uchukuzi wakati wa sikukuu ya Pasaka.
Miji mingi Marekani imeimarisha ulinzi katika viwanja vya ndege na vituo vya treni na mabasi.
Serikali hata hivyo imesema bado haina habari za uhakika kuhusu uwezekano wa kutokea kwa mashambulio Marekani.
Kundi linalojiita Islamic State (IS) limedai kuhusika katika mashambulio Brussels.

Taarifa iliyopakiwa mtandaoni na kundi hilo ilisema maeneo hayo yaliyoshambuliwa “yaliteuliwa kwa umakinifu mkubwa” na kuonya kuwa kutatokea mabaya zaidi kwa mataifa yanayopinga kundi la Islamic State.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment