Image
Image

CUF yashikilia msimamo wake wakutoshiriki uchaguzi wa marudio Zanzibar.


Zikiwa zimebaki siku mbili kufanyika kwa uchaguzi mkuu wa marudio visiwani Zanzibar chama cha wananchi CUF kimeendelea na msimamo wa kutoshiriki uchaguzi huo na kuwataka wanachama na wafuasi wa chama hicho kujiepusha na mikusanyiko isiyo ya lazima kwa kukaa majumbani mwao ili kuondokana na vurugu zinazoweza kusababishwa na wahuni dhidi ya wananchi wasio na hatia.
Akizungumza na waandishi wa habari naibu katibu mkuu wa CUF Zanzibar Bwana.Nassoro Mazrui amesema chama cha CUF hakijaweka wakala katika ngazi yoyote ya uchaguzi huo na kuwataka wafuasi kutambua swala la kupiga kura hakuna anaweza kulazimishwa.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment