Image
Image

LUBUVA:Wananchi wa Zanzibar tembeeni kifua mbele kutimiza haki yenu kikatiba.

Mwenyekiti wa wa Tume ya Uchaguzi Tanzania Jaji Damian Lubuva amewataka wananchi wa Zanzibar kutembea kifua mbele na kwenda kutimiza haki yao ya kikatiba kupiga kura hapo kesho kwa ajili ya kupata viongozi wa kuwaongoza.
Jaji Lubuva ameyasema hayo baada ya kuwepo kwa woga miongoni mwa baadhi ya wananchi kwa kuwepo kwa vikosi vya ulinzi na usalama katika maeneo mengi jambo ambalo baadhi ya wananchi wamekuwa wakihoji juu ya kuwepo kwa nguvu kubwa kiasi hicho.
''Usalama upo wa kutosha na suala la kuwepo kwa wanajeshi Zanzibar si suala geni katika mambo ya uchaguzi wa mataifa mbalimbali lengo ni kulinda amani na usalama wa wananchi hivyo wananchi wasitilie shaka wajitokeze bila uoga''-Amesema Jaji Lubuva.
Uchaguzi wa marudio Zanzibar unarudiwa kesho tarehe 20.03.2016 baada ya uchaguzi wa awali wa tarehe 25.10.2015 kufutwa na tume ya uchaguzi Zanzibar kupitia kwa Mwenyekiti wa Tume hiyo Jecha Salum Jecha kwa vigezo kadhaa kikiwepo cha upinzani kujitangazia ushindi mapema kinyume na sheria.

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment