Image
Image

Mwenyekiti na Katibu wa Chama cha Ushirika apigwa chini kwa kushindwa kutoa mchanganuo wa Korosho.

Wakulima wa Korosho Wilaya ya Masasi ,  Kata ya Sindano Mkoani Mtwara  wamelazimika  kumuondoa madarakani Mwenyekiti na Katibu wa Chama cha Ushirika cha Luatala Amcos  kwa madai ya kushindwa kutoa mchanga nuo wa malipo ya tatu ya  korosho kwa wanachama wake.
Wanachama hao wamesema wamelazimika  kuchukua hatua  baada ya viongozi hao kukaidi  agizo la  Mkuu wa Mkoa wa Mtwara ,   HALIMA DENDEGO aliyeviagiza vyama vya ushirika kuhakikisha wanakokotoa bei ya  malipo ya korosho na kuzibandika katika ofisi zao ili wakulima wafahamu mauzo ya korosho yaliyopatikana na kiasi watakachopata kama malipo ya ziada.
Wamesema pamoja na maagizo hayo ni vyama vichaache vimefanikiwa  kutimiza agizo hilo huku vyama vingine vikishindwa kufanya hivyo na ku sababisha    migogoro baina ya wakulimaa na viongozi wa vyama  vya ushirika.

Wakizungumzia migogoro hiyo watendaji wa Kata ya Likokona na Chikolopola ,CHARLES JAMES wa Chikolopola na ABASI AKITI wa Kata ya Likokokona  wamesema migogoro hiyo kwa sasa ni mikubwa baina ya viongozi wa vyama vya ushirika na wakulima na tayari taarifa hizo zimefika kwa wakuu wa wilaya ambao ni viongozi wa kamati za ulinzi na usalama ili zifanyiwe kazi.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment