Image
Image

Serikali kuipa nguvu sera ya wazee nchini kuwa Sheria.

Na Raymond Mushumbusi- MAELEZO.
SERIKALI imejipanga kuipa nguvu Sera ya wazee nchini kuwa Sheria itakayowasaidia wazee kujikwamua katika changamoto mbalimbali zinazowakabili kwa sasa.
Waziri Ummy amesema wazee wanakumbwa na changamoto nyingi katika maisha yao ya kila siku nakusema kuwa azma ya Serikali ya awamu ya Tano ni kuhakikisha wazee wanapata mahitaji yao muhimu ambayo ni huduma ya afya,haki ya kuwezeshwa kiuchumi na uwakilishi katika vyombo vya maamuzi.
“Mimi mwenyewe nalichukua jukumu hili la kufanikisha kuandikwa kwa mswaada wa Sheria ya wazee nchini na kuipeleka katika Bungeni mwezi Septemba ili tuwe na Sheria itakayowezesha kuwabana watu ambao watakaidi kutekeleza masuala yahusio wazee” Alisema Mhe.Ummy.
Naye mwenyekiti wa wazee wa mkoa wa Dar es Salaam Mzee Hemed Mkali akiwasilisha mada katika kikao hicho amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli kwa kuwajali na kuwapa kipaumbele wazee kwa kuwapa wizara ambayo itawasaidia kutatua changamoto zinazowakabili na wanaimani na Waziri husika na watashirikiana naye ili kufanya wazee wa Tanzania waishi katika maisha mazuri.
Aidha Waziri Ummy Mwalimu ameziagiza Halmashauri zote nchini katika Hospitali zilizopo chini yao kuanzisha na kuboresha madirisha kwa ajili ya wazee na kuongeza kuwa huduma kwa wazee ni bure kuanzia kumwona Daktari, Vipimo mpaka madawa na kuhamasiha wazee kuungwa kwenye Mfuko wa Afya wa Jamii (CHF) ambao unatoa huduma za afya katika maeneo mengi zaidi.

Kikao hiki cha wazee wa mkoa wa Dar es salaam na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,wazee na Watoto dhumuni kubwa ni kwa wazee ni kuomba kukutana na Mhe. Rais Dkt John Pombe Magufuli  kujadili mshtakabali wa maendeleo ya wazee nchini.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment