Image
Image

ACT- Wazalendo Wamteua Juma Saanani Kuwa Kaimu Katibu Mkuu.

HALMASHAURI Kuu ya Taifa ya Chama cha ACT- Wazalendo imemteua Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho (Zanzibar) JumaSaanani kuwa Katibu Mkuu, anaandika Pendo Omary.
Saanani anashika nafasi iliyoachwa na Samson Mwigamba huku Zitto Kabwe, Kiongozi Mkuu wa Chama hicho ikitumia Ibara ya 29 (25iv) ya Katiba ya chama hicho kumteua Mwigamba kushika nafasi ya Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Chama.
Uamuzi huo ulioridhiwa na Kamati Kuu (CC) umekuja baada ya siku tano ambapo Mwigamba alitangaza kung’oka Ukatibu Mkuu kwa kile alichokiita kwenda masomoni.
Taarifa iliyotolewa leo kwa vyombo vya habari na Ado Shaibu, Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mawasiliano kwa Umma wa chama hicho inaeleza “uteuzi wa Mwigamba umefanyika kwa kuzingatia kuwa, Mwenyekiti wa Kamati halazimika kufanya kazi Makao Makuu na hivyo Ndugu Mwigamba ataendelea na masomo yake bila kikwazo”.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment