Image
Image

Baraza la madiwani la Halmashauri ya wilaya ya Hai lawafukuza kazi watumishi sita na 5 kushushwa vyeo.


Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Hai Mkoani Kilimanjaro limewafukuza kazi watumishi wake sita na kuwashusha vyeo na mishahara watumishi watano baada ya kubainika na tuhuma za wizi, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na kuidhinisha malipo ya fedha bila idhini.
Maamuzi hayo yametolewa na baraza hilo katika kikao maalum baada ya kuridhishwa na taarifa ya kamati mbili za uchunguzi baada ya kusimamishwa kazi mwezi Novemba Mwaka Jana na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Bw.Saidi Mderu kupisha uchunguzi.
Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Bi. Helga Mchomvu amewataja waliofukuzwa kazi kuwa ni  maafisa utumishi wawili, mchumi, wahasibu wawili na dereva mmoja ambaye katika mazingira ya kutatanisha alinunua dawa hewa za Hospitali teule ya Machame yenye thamani ya shs.32.7mil.
Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri hiyo Bw Mderu amesema, tuhuma hizo ziligunduliwa na mkaguzi wa ndani wa Halmashauri yake Bw. Maiko Mosha na kufanyiwa kazi na tume hizo ambazo ziliongozwa na Bi. Grace Makiluli katibu tawala msaidizi wa sekritarieti ya mkoa wa Kilimanjaro.
Baada ya kubainika kwa tuhuma hizo baraza hilo limempongeza mkaguzi huyo  kwa kufanya kazi kwa uadilifu mkubwa kwa kuwa angeweza kudanganyika kwa kutumia fedha hizo.
Mkuu wa wilaya ya hai Bw.Gelaswus Byakanwa amelipongeza baraza hilo kwa hatua hizo  na kueleza kuwa  kazi kubwa ya Madiwani  ni kusimamia mali na raslimali za Serikali ili wananchi wapate huduma bora za serikali yao ya awamu ya tano ambayo ina dhamira ya kuwahudumia.
Source:Itv.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment