Image
Image

Breaking News:Tanzania yasaini mkataba wa Bomba la Mafuta kutoka Uganda hadi Tanga.



Serikali ya Jamhuri ya Uganda imetangaza rasmi uamuzi wake wa kutumia  bandari ya  Tanga  nchini Tanznaia kusafirishia mafuta yake ghafi kwenda nchi za nje.
Taarifa iliyotolewa na serikali jijini Dar es Salaam imesema uamuzi huo umetangazwa na Rais YOWERI MUSEVENI wa Uganda wakati wa mkutano mkuu wa 13 wa ushoroba wakaskazini uliomalizika jijini Kampala nchini Uganda.
Ujumbe wa Tanznaia uliokamilisha  mazungumzo hayo na hatimaye kushuhudia kutangazwa kwa hatua hiyo uliongozwa na Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki,Kikanda na Kimataifa DR. AUGUSTINE MAHIGA
Uongozi wa Wizara ya Nishati na Madini  unaendelea na kukamilisha  mpango huo wa bomba la mafuta ambao pia utanufaisha nchi nyingine za Afrika Mashariki na Kati.
Makamu wa Rais wa kampuni ya Total Afrika Mashariki Bwana JAVIER RIELO alishakutana na Rais JOHN MAGUFULI na wakaafikiana kwamba ujenzi wa bomba hilo linalokadiriwa kuwa la urefu wa kilomita 1,410 uanze haraka iwezekanavyo.
Kampuni ya mafuta ya Total ndiyo inayofadhili ujenzi huo na inatarajia kutumia  dola za Kimarekani karibu bilioni 4 ambazo tayari zimeshaandaliwa.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment