Image
Image

Mgomo wa daladala uliodumu kwa siku mbili mfululizo katika Manispaa ya Morogoro hatimaye umemalizika.

Mgomo wa daladala uliodumu kwa siku mbili mfululizo katika Manispaa ya Morogoro hatimaye umemalizika ambapo wananchi na madereva wameshukuru viongozi kwa kutatua tatizo hilo.
Hata hivyo wakizungumza na Radio One Stereo iliyoshuhudia daladala zikifanya  katika manispaa hiyo wakazi wa manispaa ya Morogoro  wametaka viongozi kuchukua hatua mapema kabla ya tatizo halijawa kubwa.
Wamempongeza Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dakta KEBWE STEVEN KEBWE kwa kuchukua hatua za kumsimamisha kazi Afisa wa Mamlaka ya Usafiri wa Nchi Kavu na Majini SUMATRA Mkoa wa Morogoro Bwana RAHIMU  KONDO baada ya kuonekana kulalamikiwa na madereva hao kwa kutowatendea haki.
Awali akizungumzia hatua aliyochukua kumsimamisha kazi afisa huyo wa SUMATRA Mkuu wa Mkoa wa Morogoro DR.KEBWE amesema imembidi kufanya hivyo baada ya afisa huyo kulalamikiwa na madereva kuwakamata ovyo.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment