Image
Image

Meya wa Kinondoni afuta umiliki wa vizimba 100 kwenye soko la Mawasiliano la Simu 2000.

Meya wa Manispaa ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam Mstahiki Boniface Jacob amechukua uamuzi leo wa kufuta umiliki wa vizimba na vibanda takribani miamoja vilivyokuwa vikimilikiwa na Watendaji pamoja na Madiwani wa Manispaa ya Kinondoni kwenye soko la Mawasiliano la  Simu 2000 na kuagiza wananchi wapewe bure wafanyie biashara zao.
Mstahiki Jacob aliyefuatana na watendaji wa Manispaa hiyo alitembea kwa miguu akiongea na wamachinga mmoja mmoja na makundi kuanzia Ubungo Plaza hadi Ubungo maji akiwaelimisha umuhimu wa oparesheni ya kuwaonda barabarani ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya ujenzi wa njia za juu na kuanza kwa usafiri wa mabasi ya kasi Dart ambao hali ilibadilika pale alipotaja Manispaa kuwa na masoko 26 yaliyohodhiwa na viongozi kwa kuingia Mikataba ya kupangisha wakati wamejiagawia bure.
Aidha Mstahiki Meya Boniface Jacob amesema katika kuhakikisha wafanya biashara wadogo wanatengewa maneo yao watafanya uhakiki katika masoko yote kubaini viongozi na watendaji waliojimilikisha na kuwanyang’anya ili masoko yatumiwe na walengwa ikiwa ni hatua ya kuboresha mazingira ya jiji huku mtendaji wa kata ya ubungo Bw. Gilbati Mushi akieleza hatua hiyo kudhirisha utawala bora.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment