Image
Image

Mafuriko yauwa watu watano na wengine zaidi ya 13,933 kuathiriwa wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro

Watu watano wamefariki dunia na wengine zaidi ya 13,933 kuathiriwa na mafuriko katika wilaya za Kilosa, Kilombero na Malinyi kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha mkoani Morogoro.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dk. Kebwe Stephen Kebwe amesema tathmini hiyo imetokana na mvua hizo zinazoendelea kunyesha ambapo athari nyingi zimejitokeza ikiwemo vifo, kuharibika kwa miundombinu ikiwemo barabara na madaraja pamoja na kuharibika kwa nyumba nyingi za wananchi pamoja na mashamba.
Amezitaja wilaya zilizoathirika zaidi ni Kilosa inayoongoza, Morogoro, Kilombero na malinyi ambapo jumla ya waliopoteza maisha ni wa 5,mashamba yaliyo haribika ni 12,073 nyumba 315 zimeharibika na wakazi zaidi ya 13,933 wameathirika katika kaya 3,095 kwa kukosa mahali pa kuishi na kulazimika kupata hifadhi katika maeneo ya umma na kwa ndugu,jamaa na marafiki.
Hata hivyo mbali na tathmini hiyo mkuu huyo amebainisha sababu kubwa zilizosababisha kutokea kwa mafuriko katika maeneo mengi ikiwemo katika kata ya Tindiga Manzese na msowero ni shughuli za kibinadamu ikiwemo kilimo katika maeneo ya kingo za mto mkondoa, mto Miyombo na mto Msowero hivyo kusababisha mito hiyo kujaa michanga na maji kuingia katika makazi ya watu.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment