Image
Image

Aliyekuwa kamishna ( TRA ) Harry Kitilya na wenzake warudishwa tena rumande mpaka Mei 3.

Aliyekuwa Kamishna wa TRA, Harry Kitilya, Sioi Solomoni na aliyekuwa afisa mwandamizi wa benki ya Stanbic tawi la Tanzania pia ni mshindi wa taji la Miss Tanzania 1996, Shose Sinare April 27 2016 walikosa dhamana kutokana na upande wa Jamhuri kukata rufaa mahakama kuu kupinga maamuzi ya kupewa dhamana.
Leo April 29 2016 kesi hiyo ilitajwa kusikilizwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es salaam ambapo awali Hakimu Mchauru alitoa maamuzi ya kuahirishwa kwa kesi hiyo mpaka Mei 12 mwaka huu, sababu ni kutokana na jalada halisi la kesi kupelekwa mahakama kuu baada ya kukatwa kwa rufaa ya kufutiwa shitaka namba nane la utakatishaji fedha.
Muda mfupi baadae majira ya s
aa 4;30 asubuhi walirudishwa tena mbele ya Hakimu Mchauru baada ya kupata amri kutoka kwa Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Kanda ya Dar es salaam akitamka kesi hiyo itajwe Mei 3 mwaka huu badala ya mei 12, aliyoipanga awali.
Hakimu Mchauru amesema sababu za kupewa amri hiyo hazijui, hivyo kesi itatajwa tena Mei 3 mwaka huu na yale yaliyoz
ungumzwa asubuhi yatabaki kama ilivyo, watuhumiwa wote wamerudishwa rumande.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment