Image
Image

Mwili wa Marehemu Papa wemba wawasili Kongo,kuzikwa Jumanne.

Jeneza likiwa na Mwili wa Marehemu Papa Wemba likiwa limebebwa na waombolezaji kuonekana wakilia baada ya kuwasili kutoka jijini Abidjan nchini Ivory Coast.
Baadhi ya wanenguaji wa Papa wemba wakionekana hapa na nyuma ikionekana picha Ya marehemu Papa Wemba enzi za uhai wake.
Baadhi ya vijana na wapenzi wa Muziki wa Marehemu Papa Wemba wakionekana kujichora maandishi na Picha kwenye miili yao zikimuonesha Marehemu Papa Wemba ikiwa ni sehemu ya kumuenzi.

MWILI wa mwimbaji nguli wa muziki wa dansi nchini DR Congo,Jules Shungu Wembadio Pene Kikumba (Papa Wemba), umekwisha wasili nchini humo ukitokea jijini Abidjan nchini Ivory Coast alipofariki mwishoni mwa wiki iliyopita.
Msanii huyo alipoteza fahamu akiwa jukwaani alipokuwa akitumbuiza mamia ya mashabiki na kuanguka na kukimbizwa hospitali na kufariki dunia.
Mwili wa msanii huyo tayari umewasili nchini kwao na kupokelewa na idadi kubwa ya watu katika uwanja wa ndege wa Kinshasa.
Wengi wao walionekana wakiwa wamevaa nguo zenye picha yake huku zikiwa zimeandikwa ‘Kwaheri Papa Wemba’.
Gwiji huyo wa muziki wa lingala alizaliwa mnamo Juni 14 mwaka 1949, katika eneo la Lubefu - Wilaya ya Sankuru nchini Congo.
Alikuwa maarufu katika micharazo ya muziki wa Soukous, alikuwa mmoja kati ya wanamuziki maarufu sana barani Afrika na kote duniani na mwenye sauti ya kumtoa nyoka pangoni haswa pale aimbapo akiwa jukwaani.
Papa Wemba, kama alivyofahamika na mashabiki wake, alikuwa na umri wa miaka 66 na alikuwa amepata uraia wa Ubelgiji.
Vibao vyake ni kama Mwasi,show me the way, Yolele, Mama,Proclamation"Chouchouna" (Papa Wemba), "Eluzam" na " Mbeya Mbeya" (Evoloko Lay Lay), "BP ya Munu" (Efonge Gina), "Mwana Wabi" , "Mizou" (Bimi Ombale) , "Zania" (Mavuela Somo.
Mwili wake unatarajiwa kupumzishwa katika makazi yake ya milele Jumanne ya wiki ijayo mara baada ya kuagwa siku ya Jumatatu.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment