Image
Image

Nchi zipatazo 175 zimetia saini mkataba wa Paris wa Mabadiliko ya Tabianchi.


Nchi zipatazo 175  zimetia saini kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mkataba wa Paris wa Mabadiliko ya Tabianchi ikiwa ni rekodi ya idadi kubwa ya nchi kutia saini mkataba huo mpya wa kimataifa.
Awali mataifa madogo yapatao 15 mengi yakiwa ya visiwa vidogo yalikuwa yameridhia mkataba huo lakini nchi nyingine kadhaa zilitakiwa kuchukua hatua hiyo ya pili kabla ya mkataba huo kunza kutumika.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema Mkataba wa Paris utatengeneza maisha vizazi vyote vijavyo katika njia ya aina yake kwa hatma iliyopo mikononi mwao.
Akizungumza mwanzoni mwa sherehe hiyo alisema sayari hivi sasa ilikuwa inashuhudia rekodi ya joto duniani na muda ulikuwa unakwenda kupambana na hali hiyo.

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment