Image
Image

Watu wawili akiwamo Muuguzi wa Hospitali ya Kagu wauawa kwa kukatwa mapanga kwa imani za kishirikina.


Watu wawili wameuwa kwa kukatwa mapanga sehemu mbalimabli za miili yao mkoani Geita akiwemo muuguzi wa Zahaati ya kagu kwa kile kinachodaiwa kwa imani za kishirikina.
Tukio la kwanza limetokea juzi majira ya saa moja jioni ambapo Helena Paulo 56 mkazi wa kijiji cha Luhuma alikatwa mapanga wakati akiwa njiani kuelekea nyumbani kwake huku Elizabeti Masango 54 ambaye ni muuguzi wa Zahanati naye alikatwa mapanga akiwa nyumbani kwake.
Wakizungumza mashuhuda wa matukio hayo wamesema vitendo vya uhalifu wa kukatwa mapanga akinamama vinaongezeka
mkoani Geita, jambo linalowafanya kuishi kwa mashaka.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Geita Ali Kidwaka aliyekwenda kutoa pole kijijini Kagu amewataka wananchi kuwafichua watu wanaofanya unyama huo huku mwenyekiti wa kijiji hicho Tanga Daudi amessitiza ulinzi mkubwa wa jadi umeimarishwa kila kona.
Kamanda wa Polisi Mkoani Geita Mponjoli Mwabulambo amesema mtu mmoja anashikiliwa kwa mahojiano kufuatia matukio hayo.
 

Source:Channel Ten.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment