Image
Image

Serikali imesema bado ugonjwa wa Malaria ni tatizo kubwa katika jamii.

Serikali imesema bado ugonjwa wa malaria ni tatizo kubwa katika jamii hivyo inafanya kila liwezekanalo kuhakisha mapambano dhidi ya ugonjwa huo yanaongezewa nguvu ili kuokoa watu wanopoteza maisha kutokana na Malaria.
Hayo yameelezwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee  na Watoto katika hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na Mkurugenzi wa Huduma na Kinga katika wizarahiyo DK NEEMA RUTH BEMAHILA wakati wa  matembezi maalum ya kilomita tano ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya malaria duniani.
Katika maadahimisho hayo kulizinduliwa filamu fupi ya namna ya kujikinga na ugonjwa wa malaria ambayo itatumiwa kama moja ya nyenzo zitakazosaidia kuhimiza vita dhidi ya malaria hapa nchini.
Nao waratibu wa matembezi hayo wamesema mwitikio umekuwa mzuri na kwamba jambo muhimu ni serikali kuongeza nguvu katika vita hivi kwani malaria inaepukika.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment