Image
Image

Kesi ya BOSI TRA Harry Kitilya na wenzake kusikilizwa May 5 2016.

Aliyekuwa Kamishna wa TRA, Harry Kitilya, Sioi Solomoni na aliyekuwa afisa mwandamizi wa benki ya Stanbic tawi la Tanzania pia ni mshindi wa taji la Miss Tanzania 1996, Shose Sinare April 27 2016 walikosa dhamana kutokana na upande wa Jamhuri kukata rufaa mahakama kuu kupinga maamuzi ya kupewa dhamana.April 29 2016 kesi hiyo ilitajwa kusikilizwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es salaam ambapo awali Hakimu Mchauru alitoa maamuzi ya kuahirishwa kwa kesi hiyo mpaka Mei 12 mwaka huu, sababu ni kutokana na jalada halisi la kesi kupelekwa mahakama kuu baada ya kukatwa kwa rufaa ya kufutiwa shitaka namba nane la utakatishaji fedha.
Muda mfupi baadae majira y
a saa 4;30 asubuhi walirudishwa tena mbele ya Hakimu Mchauru baada ya kupata amri kutoka kwa Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Kanda ya Dar es salaam akitamka kesi hiyo itajwe Mei 3 mwaka huu badala ya mei 12, aliyoipanga awali.
Sasa Leo 3 May 2016 ambapo Mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu Dar es salaam ilipanga kusikiliza kesi hiyo kutokana na jalada halisi la kesi kupelekwa mahakama kuu kurudi leo lakini halijarudi hivyo kesi hiyo imeahirishwa mpaka Mei 18 2016 watuhumiwa wamerudishwa rumande.
Hata hivyo watuhumiwa walitakiwa kufika mahakama Kuu kwa ajili ya kuendelea na rufani ambapo baada ya k
ufika Mahakama Kuu kanda ya Dar es salaam imepanga kuanza kusikiliza rufani hiyo May 5 2016.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment