Image
Image

Taifa Stars yalazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya wenyeji Kenya Harambee Stars.

TIMU ya soka ya Taifa (Taifa Stars) imelazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya wenyeji Kenya (Harambee Stars) katika mechi ya kirafiki ya kimataifa iliyofanyika jana kwenye Uwanja wa Moi Kasarani jijini hapa.
Stars ikicheza bila ya nahodha wake Mbwana Samatta wa KRC Genk ya Ubelgiji na Thomas Ulimwengu wa TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), ilikuwa ya kwanza kupata bao katika dakika ya 32 lililofungwa na straika wake Elius Maguli kwa kichwa baada ya kuunganisha krosi safi ya Juma Abdul.
Timu zote zilikuwa zinashambuliana kwa zamu na dakika sita baadaye Harambee Stars walisawazisha bao hilo kupitia kwa mchezaji wake Victor Wanyama anayeichezea klabu ya Southampton ya Ligi Kuu ya England kwa njia ya penalti.
Refa wa mchezo huo, Brian Nsubuga kutoka Uganda alitoa penalti hiyo baada ya mshambuliaji wa Harambee Stars, Humphrey Ochieng kuangushwa kwenye eneo la hatari na mabeki wa Taifa Stars.
Katika mchezo huo Stars ilianza mchezo kwa taratibu lakini ilimaliza kwa kasi na kuwapa wakati mgumu wapinzani wao.
Kiungo Jonas Mkude alimfunika kabisa Wanyama ambaye alionekana tu wakati anaifungia kwa penalti ya utata timu yake bao la kusawazisha.

Kocha wa Stars, Boniface Mkwasa aliwatumia wachezaji wake wengi aliowaita kwa mara ya kwanza kwa ajili ya kujiandaa kuivaa Misri (The Pharaos) Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Kipindi cha pili kilipoanza Mkwasa alifanya mabadiliko kwa kumtoa kipa Deogratius Munishi 'Dida' na nafasi yake kuchukuliwa na Aishi Manula na huku Mkude na Elius Maguli nao wakitoka na nafasi zao kuchukuliwa na Mohamed Ibrahim na Jeremiah Juma.
Vikosi vilivyokuwa:
Kenya; Boniface Oluoch, Joakins Atudo, Abud Khamis, Eugene Asike, David Owino, Anthony Akumu/Ally Abondo (dk 78), Victor Wanyama, Ayub Timbe/ John Makwatta, Humphrey Mieno/ Cliford Miheso (dk 56), Eric Yohanna na Jesse Were/ Wycliff Ochomo (dk70).

Stars; Deogratius Munishi ‘Dida’/Aishi Manula (dk 62), Juma Abdul, Mohamed Hussein ‘Tshabalala’, Aggrey Morris, Erasto Nyoni, Jonas Mkude/ Mohammed ‘Mo’ Ibrahim (dk 62), Himid Mao, Shiza Kichuya, Mwinyi Kazimoto, Elias Maguli / Jeremiah Juma (dk 83) na Deus Kaseke/ Farid Mussa (dk 65).
    Share on Google Plus

    Kuhusu TAMBARARE HALISI

    This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

    0 comments:

    Post a Comment