Image
Image

5 wauawa Bekaa 15 wajeruhiwa katika mfululizo wa mashambulizi.

Watu watano wameuawa na wengine 15 wamejeruhiwa mapema Jumatatu asubuhi katika mfululizo wa mashambulizi ya kujitoa mhanga katika kijiji cha mashariki mwa Libanon karibu na mpaka na Syria, viongozi wametangaza.
Mfululizo huu wa milipuko ume
tokea katika kijiji cha Qaa, kinachokaliwa na watu kutoka jamii ya Wakristo, katika jimbo la Bekaa, karibu na mpaka na Syria.
Mashambulizi haya manne ya kujitoa mhanga yametokea kwa muda wa dakika chache katika kijiji cha Qaa, katika jimbo la Bekaa. Mshambuliaji wa kwanza wa kujitoa mhanga amelipua mkanda wake uliokua umejaa vilipuzi katika eneo la kituo cha ukaguzi cha jeshi la Lebanon. Wakati watu walipokua wakikimbia kuwaokoa waathirika, mgaidi mwingine alijilipua, akifuatiwa na washambuliaji wawili wakujitoa mhanga.
Hakuna kundi hata moja ambalo limeshatangaza kuhusika na mfululizo huu wa mashambulizi, lakini kwa vyovyote vile kundi la Islamic State linanyooshewa kidole kwa kuhusika na tukio hilo. Kwa sababu wanajihadi wa kundi hili linaloongozwa na Abu Bakr al-Baghdadi, wanaendesha mara kwa mara harakati zao katika jimbo hili lenye milima, kunakopatikana kijiji cha Qaa.
Wakati huo huo wa mashambulizi ya Qaa,kundi la Islamic State limekua likiendesha mashambulizi kababmbe dhidi ya kijiji cha Brital kinachokaliwa na watu kutoka jamii ya Mashia, lakini wapiganaji wa kundi hili walirudishwa nyuma na jeshi la Lebanon baada ya mapigano makali. Mapigano kati ya jeshi la Lebanon na kundi la Islamic State yanatokea mara kwa mara kwenye umbali wa kilomita 50 kwenye mpaka wa Lebanon na Syria, katika eneo kulikojengwa makambi kadhaa ya wakimbizi wa Syria.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment