Image
Image

Ujumbe wa baraza la amani na usalama wa umoja wa Afrika, wamaliza ziara yake Burundi

Ujumbe wa baraza la amani na usalama wa umoja wa Afrika uliofanya ziara nchini Burundi, umehitimisha ziara yake mwishoni mwa juma, ambapo umesema, licha ya hali kuimarika, bado kuna mengi ya kufanywa kwenye taifa hilo.
Wakizungumza na wandishi wa habari mjini Bujumbura baada ya kumaliza ziara ya siku 2, wajumbe hao wa baraza la amani na usalama la umoja wa Afrika, wamebaini kuwa wamekusanya habari zote walizokuwa wakihitaji na kwamba watatoa maagizo wakifika Addis Ababa.
Mmoja wa wajumbe walio
tembelea nchi hiyo, Makayate Safouesse anasema ziara yao imewasaidia kujua namna hali ya mambo ilivyo nchini Burundi, na kwamba watakaporejea mjini Addis Ababa watakuwa na mengi ya kueleza kwa wakuu wa nchi.
Ama kuhusu mazungumzo baina ya warundi yanayofanyika mjini Arusha chini ya usuluhishi wa rais wa zamani wa Tanzania, Benjamin Mkapa, amesema ikiwa muungano wa upinzani CNARED na makundi mengine wataweza kushiriki, huenda suluhu ikapatikana mapema zaidi.
Safousesse, amesema ni jukum
u la msuluhishi kuzialika pande anazoona zinahusika na zina umuhimu mkubwa kwenye kupata suluhu ya nchi hiyo, na kwamba ikiwa ameona inafaa kuzialika pande ambazo hazikushiriki awali, ni jambo jema.
Ziara hii imefanyika wakati awamu nyingine ya mazungumzo baina ya wadu wa siasa,
Burundi yanatarajiwa kuitishwa mjini Arusha Tanzania mwanzoni mwa mwezi ujao, yote hayo ikiwa ni katika lengo la kutaka kuumaliza mzozo wa kisiasa unaoikabili Burundi, ambao umedumu kwa mwaka mmoja sasa.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment