Image
Image

Sababu za MELI ya Mizigo ya Mv. Happy kuzama bahari ya hindi hizi hapa.

MELI ya Mizigo ya Mv. Happy iliyokuwa ikitokea Dar es Salaam kwenda  Zanzibar  imezama katika Bahari ya Hindi   ikiwa imebeba mbao zaidi ya 1090 na magunia 450 ya viazi mviringo.
Hata hivyo,  mabaharia 12 ambao ni wafanyakazi katika meli ya mizigo  ya hiuo wamesalimika kufa maji  kwa vile meli hiyo  haikuzama yote  katika eneo la Kizingo  kisiwani Zanzibar.
Tukio hilo lilitokea jana alfajiri kisiwani Unguja.
Mkuu wa Operesheni baharini, Msilimiwa Idd,  alisema tukio hilo lilitokea saa 8.00 usiku baada ya meli hiyo kuyumba kutokana na dhoroba kali ya upepo.
Alisema ilipotimu saa saa 9.00usiku nahodha wa meli hiyo  alipoona hali imezidi kuwa mbaya akaelekea katika Kisiwa Mchanga  ambako alijikuta akikwama kwa vile upande mmoja wa meli ulikuwa unapitisha maji.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment