Image
Image

Kisanduku cha EgyptAir chakarabatiwa.

Kisanduku kimoja kati ya viwili vya kurekodia data vya ndege ya Misri iliyoanguka katika Bahari ya Mediterania mwezi uliopita kimekwishakarabitiwa, imesema kamisheni ya uchunguzi hii leo, na kuzusha matumaini kuwa kinaweza kutoa fununu ya chanzo cha ajali ya ndege hiyo.
Visanduku hivyo vilipatikana wiki mbili zilizopita, lakini vilikuwa vimeharibika vibaya kiasi cha kutoweza kutoa taarifa yoyote kuhusu ajali hiyo, iliyoangamiza watu wote 66 waliokuwa katika ndege hiyo iliyokuwa safarini kutoka Paris kuelekea Cairo.
Kamisheni hiyo ya uchun
guzi iliyoko mjini Paris imesema imefanya majaribio, na inao uhakika kuwa visanduku hivyo vilirekodi kikamilifu utaratibu wa safari ya ndege iliyoanguka. Hali kadhalika imesema kuwa kazi ya kukirabati kisanduku cha pili itaanza kesho.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment