Image
Image

Messi astaafu soka, Argentina aangukia pua Copa Amerika.

Katika hatua iliyoonekana kuwashanga wapenzi wa soka nchini Argentina na dunia kwa ujumla, mshambuliaji wa klabu ya Barcelona na timu ya taifa ya Argentina, Lionel Messi, ametangaza kustaafu kuichezea timu yake ya taifa.
Uamuzi wa Messi kustaafu
kucheza soka la kimataifa, umewachukua watu kwa mstuko, hasa ikiwa ni baada ya timu yake ya taifa kushindwa kutwaa taji la michuano ya Copa Amerika.
Mchezaji huyo na timu yake ya taifa kwa mara nyingine walishindwa kufua dafu katika ngazi ya kimataifa, ikiwa ni mara ya nne mfululizo kwa mchezaji huyu akiwa na timu yake ya taifa kushindwa kutwaa taji lolote kubwa baada ya hapo jana timu ya taifa ya Chile kuchomoza na ushindi kwa njia ya penati.
"Kwangu mimi, timu ya taifa nimemaliza," alisema Lionel Messi wakati akizungumza na waandishi
wa habari baada ya mechi na Chile.
"Nimefanya kila nilichoweza, nimeshiriki fainali nne, inauma kushindwa kuwa bingwa, ni wakati mgumu kwangu na timu nzima pia, na ni ngumu kusema, lakini nimemalizana na timu ya taifa ya Argentina." alisema Messi.
Uamuzi huu wa kushanga wa Lionel Messi umekuja baada ya kushindwa kwenye fainali ya tatu mfululizo akiwa na timu ya taifa, toka kwenye fainali za kombe la dunia nchini Brazil, mwaka 2014.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment