Image
Image

Milovan ateuliwa kuwa kocha mkuu wa timu ya Algeria

Shirikisho la soka nchini Algeria, limemteua aliyekuwa kocha mkuu wa timu ya taifa ya Ghana, Milovan Rajevac, kuwa kocha wake mkuu mpya wa timu ya taifa.
Rajevac mwenye umri wa miaka 62 hivi sasa, anakuwa kocha wa kudumu wa kikosi hicho cha mbweha wa jangwani, akiziba nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa kocha mkuu wa timu hiyo, Christian Gourcuff aliyejiuzulu nafasi yake mwezi April mwaka huu.
Rajevac aneyfahamika zaidi barani Afrika wakati akiifundisha timu ya taifa ya Ghana, ambayo aliion
goza kufika hatua ya nusu fainali timu yake ikipoteza kwa mikwaju ya Penati kwenye fainali za kombe la dunia nchini Afrika Kusini mwaka 2010.
Kocha huyu raia wa Serbia, pia aliwahi kukinoa kikosi cha timu ya taifa ya Qatar.
Shirikisho la mpira la Algeria lilimtangaza Rajevac kuwa kocha mkuu wa timu ya taifa na kuongeza kuwa kocha huyo atawasili nchini humo katikati ya mwezi july ambapo atatangazwa rasmi kwa vyombo vya habari.
Hakuna taarifa zaidi zilizotolewa kuhusu mkataba wa kocha huyu, ingawa ni wazi inaonekana atakuwa na jukumu la kukiongoza kikosi hicho kwenye mechi za kufuzu kucheza fainali za kombe la dunia nchini Urusi,mwaka 2018.
Timu ya taifa ya Algeria iko kwenye kundi B sambamba na timu ya taifa ya Nigeria, Cameroon na Zambia, mechi hizi zinatarajiwa kuanza kupigwa mwezi October mwaka huu.
Rajevac pia atakiongoza kikosi hicho kwenye fainali za kombe la mataifa ya Afrika mwakani nchini Gabon.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment