Image
Image

Mwanahabari Mkongwe Alfred Masako Astaafu taaluma ya Habari.

 Alfred Masako -Mwandishi wa habari Mkongwe na wasiku nyingi nchini Tanzania

Mwandishi wa habari Mkongwe na wasiku nyingi nchini Tanzania Alfred Masako ametangaza kustaafu maswala ya Taaluma ya habari baada ya kufanya kwa miongo ishirini na Mitatuu sasa. 
Mwanahabari huyo amesema kuwa kwa muda ambao amefanya kazi ya uandishi wa habari na utangazaji umefika muda wa yeye kupumzika kusudi na wengine nao wafanye kazi hiyo, kwani kila uchao taaluma inakuwa na watu nao wanaongezeka hivyo ni wakati muafaka kwake kupumzika kwani pia hata umri umeenda.
Bwana Masako ambaye ametumikia ITV/Radio One ambacho ni kituo kikubwa nchini Tanzania amekuwa nimoja ya mtangazaji mwenye mvuto wa kipekee haswa anapokuwa akiripoti habari ama kufanya matangazo ya moja kwa moja kutoka eneo moja mpaka lingine,haswa ikikumbukwa tukio la lori la mafuta lililokuwa limepata ajali na mafuta kumwagika,Akisema Mwenye kikombe hayaaa,mwenye kijiko hayaa.
Uamuzi wa kustaafu Taaluma ya Habari kwa Bwana.Masako ameuweka wazi wakati wa Sherehe za ITV/Radio One ambazo nizakila Mwaka zenye kukutanisha wafanyakazi wa Kampuni hiyo kwalengo la kufahamiana na kufurahi pamoja na viongozi wao wajuu ili kuweza kupata morali ya kufanya kazi kwa bidii zaidi, hivyo kumuaga Mwanahabari huyo Nguli katika taaluma ya Habari.
Bwana Masako amesema kwamba amefarijika kwa Kampuni na wafanyakazi wenzake kutambua mchango wake na kufanya uamuzi wa kumuaga wakati wa sherehe hiyo kwani linaonesha kuwa na umoja na mshikamano kazini.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa ITV/Radio One Joyce Mhavile amesema kuwa kustaafu kwa Bwana.Masako nijambo jema lakini bado watamkumbuka sana tu kwani amekuwa ni mwanahabari wa Muda mrefu katika kituo hicho na amekuwa na mchango wa kuigwa,huku akijaribu kulizia sauti yake kama alivyokuwa akiripoti katika matukio kadhaa huku akionesha Tabasamu usoni kwa kumaanisha ni mwenye furaha.  
Aidha katika Sherehe hiyo walialikwa wasanii maarufu akiwamo Ali Kiba Msanii wa Bongo Flava nchini Tanzania pamoja na msanii wa Tamthilia kutoka nchini Afrika Kusini Sisa Hewana maarufu kama Skumbuzo wa ISIDINGO the NEED.
Wafanyakazi na wawakilishi kutoka mikoani na Visiwani Zanzibar walijumuika katika sherehe hiyo ya mwaka, nakuonesha vipaji vyao vya kuimba na kusakata rumba. 

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment