Image
Image

Raia 18 wauawa katika mripuko Somalia

Raia wasiopungua 18 wameuawa baada ya basi dogo lililojaa abiria kuripukiwa na bomu lililotegwa kandoni mwa barabara, katika mji wa Lafole, kusini-magharibi mwa mji mkuu wa Somalia Mogadishu. Hakuna kundi lililojitokeza mara moja kudai kuhusika na shambulio hilo, lakini wapiganaji wa Al-Shabaab wamekuwa wakifanya mashambulio ya mara kwa mara dhidi ya vikosi vya usalama na raia nchini kote katika siku zilizopita. Afisa wa polisi Abidkadir Mohamed, amesema bomu hilo limeripuriwa kwa kutumia rimoti, na kwamba watu wote waliokuwemo ndani ya basi wameuawa na kuteketea. Nur Ahmed, ambaye alikuwa akiendesha gari kwenye barabara ulipotea mripuko huo, amesema basi hilo dogo lilikuwa likisindikizwa na gari lililowabeba wanajeshi, ambalo yumkini ndilo lililokuwa limelengwa na mripuko huo.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment