Image
Image

Machinjio Manispaa ya Morogoro ni kero kwa wakazi na wafanyabiashara.

Na,Devotha Songorwa,Morogoro.    ..................................................................................................................................
Machinjio ya Manispaa ya Morogoro yameendelea kuwa kero kwa Wafanyabiashara na wakazi wa eneo hilo kutokana na kutiririsha maji taka kwenye mitaro ya maji ya mvua kwa muda mrefu.
Wafanyabiashara hao, Bi.
Mushi Ally na Dismas Layoze wamesema machinjio hayo yamekuwa kero kwao na hata wapita, njia kutokana na harufu kali inayotokana na maji taka kutoka machinjioni kutiririshwa na kuingia kwenye mifereji ya maji ya mvua kando ya barabara iendayo mjini kutoka Msavu.
Wamesema hali hiyo ipo kila siku na kusababisha eneo hilo kuwa na mazingira machafu, hivyo kuwa tishio la kuwepo kwa magonjwa mlipuko ukiwemo ugonjwa wa kipindupindu.
Aidha wamesema wameiomba idara ya afya manispaa ya Morogoro kulishughulikiea suala hilo, ili kulinda afya ya wananchi wanaoishi na kufanya biashara zao katika eneo hilo.
Like ukurasa wetu wa Facebook,Instagram,Twitter,kupata habari zinapotufikia.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment