Image
Image

Merkel kuzungumzia sera yake ya wakimbizi.

Kansela Angela Merkel atafanya mkutano wake wa kila mwaka na waandishi habari leo kufuatia mashambulizi kadhaa, ambayo yameitikisa Ujerumani na kuzusha maswali juu ya sera yake ya kufungua milango kwa wakimbizi.
 Merkel alilazimika kukatiza likizo yake ya majira ya joto na anafanya tukio lake hilo la kila mwaka mapema kuliko ilivyopangwa.
Mashambulizi matatu kati ya manne tangu Julai 18 yalifanywa na watu wanaoomba hifadhi, na mawili kati ya hayo wanamgambo wa kundi la itikadi kali la Dola la Kiislamu walidai kuhusika .
Mashambulizi hayo yaliyodaiwa kufanywa na kundi la Dola la Kiislamu ni pamoja na shambulio na kisu na shoka katika treni jimboni Bavaria, shambulio la risasi mjini Munich, shambulio la kisu mjini Reutlingen na shambulio la bomu la kujitoa muhanga mjini Ansbach.
Umaarufu wa Merkel umeporomoka mapema mwaka huu kuhusiana na wasiwasi juu ya wakimbizi milioni 1.1 waliowasili nchini Ujerumani mwaka 2015, lakini ulipanda tena baada ya kura nchini Uingereza ya kujitoa kutoka Umoja wa Ulaya mwezi Juni na jaribio la mapinduzi nchini Uturuki mapema mwezi huu.
Sera kuhusu wakimbizi
Mtu kutoka Syria ambaye alikuwa anaomba hifadhi ya ukimbizi aliwajeruhi watu 15 siku ya Jumapili alipojiripua nje ya ukumbi wa tamasha la muziki katika mji wa kusini nchini Ujerumani wa Ansbach, alikuwa arejeshwe nchini Bulgaria zaidi ya mwaka mmoja uliopita.
 Mashambulizi hayo yameamsha mjadala juu ya vipi kushughulikia waombaji hifadhi ambao ni wahalifu na juu ya kuweka ulinzi katika mipaka ya Ujerumani.
Maafisa katika jimbo la Bavaria, ambako mashambulizi yalitokea, wanatoa wito kwa wakimbizi kufanyiwa uchunguzi mkali na wa kina pamoja na kubadilishwa kwa sera ya serikali kutowarejesha wakimbizi walikotoka katika maeneo ya mizozo.
Merkel amekuwa mara kwa mara akisisitiza kwamba mipaka ya Ujerumani itabakia wazi na kwamba uhalifu unaofanywa na watu wachache wanaoomba hifadhi haupaswi kusababisha shaka kwa watu wote ambao ni wakimbizi.
Makundi ya siasa kali
Ghasia za hivi karibuni zimeleta msuguano wa kisiasa ndani ya kundi lake la wahafidhina juu ya ahadi yake ya kuwapa hifadhi wale wote wanaokimbia vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Syria.
Kundi la chama cha siasa kali za mrengo wa kulia nchini Ujerumani la Alternative for Germany, chama mbadala kwa Ujerumani, AfD limetumia ongezeko la matukio haya ya matumizi ya nguvu kumshutumu Merkel kwamba anaifanya nchi hii kuwa lengo la mashambulizi.
Kiongozi huyo wa Ujerumani pia anatarajiwa kuelezea juu ya ghasia zilizotokea nchini Uturuki kufuatia jaribio la mapinduzi mapema mwezi huu na athari zake katika makubaliano juu ya wahamiaji kati ya Umoja wa Ulaya na Uturuki.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment