Image
Image

Waliohusika kumtesa kinyama kijana Mtanzania kwenye mgodI wa Nyamahuna wanaswa.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,  MWIGULU NCHEMBA   ameagiza wale wote walioshiriki kumpiga na kumfungia  kwenye konteina   kijana   MASANJA SHOKAA   kuwekwa  chini ya ulinzi ili kulisaidia jeshi la polisi.
Ametoa agizo hilo alipotembelea   mgodi wa Nyamahuna unaomilikiwa na raia kutoka China uliopo Wilayani Geita unaodaiwa kuwa na tabia ya kutesa na kuua wafanyakazi wake.
Picha za mateso ya wafanyakazi katika mgodi huo kwa muda wa wiki moja sasa zimekuwa zi kisambazwa katika mitandao ya  jamii .
Kijana SHOKAA aliyekuwa mfanyakazi wa kampuni hiyo ya uchimbaji dhahabu alidaiwa kufung i wa ndani ya kontena na kupigwa kwa magongo na fimbo mpaka alipozimia na hatimaye kufikishwa kituo cha polisi kufunguliwa mash i taka ya wizi.
Waziri NCHEMBA amesema  uchunguzi wa awali unaon esha kumekuwepo na tabia ya kuwabambikizia kesi wafanyakazi wanaoonekana mstari wa mbele kudai maslahi yao
Katika  hatua nyingine  imebainika kuwa katika mgodi huo kuna wahamiaji haramu zaidi ya  50  huku kukiwa na vibali ishirini na  vi nane vya ra ia wa China walioingia nchini kwa njia  halali .
Kupitia kwenye ukurasa wake wa Facebook waziri wa mambo ya ndani ya nchi Mwigulu Nchemba ameandika haya.

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment