Image
Image

Ufinyu wa bajeti waigharimu MOI kuzidiwa na wagonjwa.


Dar es Salaam. Ufinyu wa bajeti katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa (MOI) umesababisha taasisi hiyo kuzidiwa na wagonjwa wa upasuaji, huku wengine wakisubiri huduma hiyo kwa zaidi ya miezi minne.
Kabla ya tatizo hilo la kifedha MOI ilianzisha kambi maalumu ya Jumamosi na Jumapili na waliweza kuhudumia wagonjwa hadi 30 kwa siku hizo mbili.
MOI kwa kawaida hutoa huduma ya upasuaji kwa wagonjwa wanane hadi 10 kwa siku, lakini kutokana na ufinyu wa bajeti uliosababisha kuondolewa kambi za mwishoni mwa wiki, umesababisha ongezeko la idadi kubwa ya wagonjwa wanaohitaji upasuaji.
Uchunguzi uliofanywa na Mwananchi katika wodi ya MOI jengo jipya, umebaini uwapo wa idadi kubwa ya wagonjwa waliokaa muda mrefu wakisubiri huduma ya upasuaji, huku wengine wakirejeshwa nyumbani.



Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment