Image
Image

Abu Muhammed Al-Adnani auawa kwenye mapigano yaliyotokea Aleppo nchini Syria

Msemaji wa kundi la kigaidi la DAESH Abu Muhammed Al-Adnani, ameripotiwa kuuawa kwenye mapigano yaliyotokea Aleppo nchini Syria.Taarifa hizo za kifo cha msemaji huyo zilitolewa na shirika la habari la Amak lenye uhusiano wa karibu na DAESH.
Kwa mujibu wa taarifa hizo, Al-Adnani alikuwa amekwenda mjini Aleppo kwa ajili ya kukagua operesheni zilizopangwa dhidi ya wanajeshi.
Kwa upande mwingine, idara ya ulinzi ya Marekani ya Pentagon ilitoa maelezo na kuarifu kwamba ndege za kivita zilitekeleza operesheni iliyomlenga Al-Adnani ingawa maelezo zaidi hayakubainisha iwapo aliuawa.
Al-Adnani mwenye umri wa miaka 39 ambaye jina lake la asili ni Twaha Subhi Fellaha, anatambulika kuwa na uhusiano wa karibu na kiongozi wa DAESH Abubakar Al-Baghdadi.
Kwa mara ya mwisho Al-Adnani alionekana mwezi Mei akitoa wito wa mashambulizi dhidi ya magharibi kwenye kanda ya video aliyorekodi.
Mnamo tarehe 5 Mei 2015, Idara ya ulinzi ya Marekani ilitangaza tuzo ya fedha dola milioni 5 kwa yeyote atakayetoa taarifa zitakazosaidia kumkamata Al-Adnani .
Takriban miaka 3 sasa mji wa Aleppo umekuwa ukikumbwa na mizozo kati ya vikosi vya upinzani na wanajeshi wa serikali ya utawala nchini Syria.

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment