Image
Image

Afisa wa polisi ashambuliwa kwa kisu mjini Toulouse nchini Ufaransa

Afisa mmoja wa polisi ameripotiwa kujeruhiwa baada ya kushambuliwa kwa kisu katika mji wa Toulouse kusini mwa Ufaransa.Katibu mkuu wa polisi nchini Ufaransa Didier Martinez alitoa maelezo na kuarifu kutekelezwa kwa shambulizi hilo dhidi ya afisa wa polisi kwenye kituo cha Toulouse mtaani Rempart Saint-Etienne.
Maelezo zaidi yanaarifu kwamba mshambuliaji aliingia kituoni kwa kudanganya kutaka kuwasilisha kesi ambapo ghafla akachomoa kisu na kumshambulia afisa wa polisi huku akitaka kumpora bastola.
Afisa huyo wa polisi alipata majeraha madogo kwenye makabiliano na mshambuliaji.
Idara ya polisi imeripoti kumtia mbaroni mshambuliaji huyo na kuanzisha uchunguzi ili kubainisha endapo tukio hilo linahusiana na ugaidi.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment