Image
Image

Rais Erdogan ajumuika pamoja na familia za mashujaa ikulu

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan alijumuika pamoja na familia za mashujaa ikulu kwa ajili ya chakula cha jioni.
Erdogan alisema kwamba kundi la FETO linaloongozwa na Fethullah Gulen lilikuwa na lengo la kuiteka Uturuki na dunia nzima kwa ujumla.
Akibainisha kuendeleza mapambano yake dhidi ya FETO, Erdogan alisema, ‘’Yeyote anayeendelea kujihusisha na kundi la FETO ni mhaini.’’
Rais Erdogan pia alitoa wito kwa wananchi wote kutoa taarifa kwenye mamlaka husika endapo watagundua taasisi zozote zinazojihusisha au kuendeshwa na wafuasi wa kundi i la FETO.
Erdogan pia alikumbushia kwamba makundi ya kigaidi yanapokea misaada na kuunga mkono na magharibi.
Erdogan alionya kwamba matatizo yanayoikumba Uturuki kwa sasa huenda yakaikumba magharibi kutokana na harakati za kigaidi endapo mapambano dhidi yao yatafifia.
Wakati huo huo, mawasiliano kwa njia ya video yalifanyika kati ya Erdogan na afisa mkuu wa operesheni za Jerablus Efe Trabzon.
Afisa huyo alifahamisha kuendelezwa vyema kwa operesheni ya Firat bila ya matatizo yoyote na kuwataka wananchi kuondoa hofu.
Erdogan naye alisema, ‘‘Nina furaha kubwa kupata fursa ya kujumuika pamoja na familia za mashujaa wetu. Tunafuatilia kwa makini harakati za kijeshi na operesheni za usalama zinazoendelea Jerablus. Mola atusaidie.’’
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment