Image
Image

Idadi ya watu waliofariki kwenye shambulizi la bomu lililotekelezwa mjini Mogadishu yafikia 10

Idadi ya watu waliofariki kwenye shambulizi la bomu lililotekelezwa karibu na maeneo ya ikulu ya rais katika mjini mkuu wa Mogadishu nchini Somalia imeripotiwa kufikia 10.Shambulizi hilo lililolenga hoteli moja iliyoko eneo hilo lilisababisha uharibifu mkubwa.
Baadhi ya wanasiasa pamoja na mawaziri wa serikali walikuwa wakifanya mkutano wa usalama ndani ya hoteli hiyo.
Watu 30 akiwemo waziri mmoja wa serikali wameripotiwa kujeruhiwa kwenye shambulizi hilo.
Kundi la Al-Shabaab linalohusiana na Al-Qaeda limetangaza kutekeleza shambulizi hilo.
Serikali ya Uturuki imekemea na kulaani shambulizi hilo.
Wizara ya mambo ya nje ya Uturuki imetoa maelezo na kuarifu kusimama pamoja bega kwa bega na Somalia ili kurudisha amani na utulivu nchini.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment