Image
Image

CHADEMA yaubomoa UKUTA wake kwa Mwezi mmoja.

Na.Salum Msangi,Dar es Salaam. 
Maandamano yaliyokuwa yamepangwa kufanywa nchi nzima na Chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA yaliyokuwa yanafahamika kwa jina la UKUTA yamesitishwa kwa muda wa Mwezi mmoja.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa CHADEMA Mh.Freeman Mbowe amesema kuwa wameamua kuahirisha maandamano hayo mara baada ya kuombwa na viongozi wa dini nchini.
"Mimi ni miongoni mwa watu ambao tulitamani kesho watu wawe barabarani, wanachama wetu ambao watakwazika, UKUTA sio CHADEMA, UKUTA ni mchanganyiko wa makundi mbalimbali ya watanzania. Sasa hayo makundi yamekuja kutushauri tuwe pamoja, sisi ni nani tukatae. Watu kama Mwl Nyerere foundation wametusihi, hata Lowassa amaengea na mama Maria Nyerere wametusihi."Mbowe.
Mh.Mbowe amesema kuwa uamuzi huo wa kusitisha maandamano hayo ya UKUTA nchi nzima yamewapa wakati mgumu kwakuwa sio kila kitu kinachoamuliwa kinawapendeza wanachama, lakini anaamini kuwa wanachadema watatuelewa kwa hili.
"Sio kila wakati viongozi tutafanya mambo yatayowapendeza wanachama wetu, Viongozi wa dini awali walikuja na ajenda moja, kuomba wabunge wa UKAWA warejee bungeni, Kamati kuu ya CHADEMA imepokea kwa heshima sana wito wa viongozi wa dini.
Kufuatia harakati za Operesheni UKUTA ambazo zimekuwa zikiendendelea kwaajili ya kufanikisha azma yao, Mbowe amesema kwa Mpaka jana wamekuwa na viongozi 230 amabao wameshtakiwa, huku viongozi 28 mapaka jana wakiwa hawajaachiwa kwa mujibu wa takwimu walizonazo wakijumuisha na Naibu katibu mkuu Zanzibar Salum Mwalimu.
Hata hivyo mbowe amesikitishwa na kitendo cha watu ambao anawaita ni Mahasimu wao ambao wamekuwa wakijaribu kuwagombanisha ndani ya CHADEMA.
" Hizi fitna za mitandao mbowe sina tabia ya kutoa matakamko nje ya taratibu za chama, Tamko nililotoa ni la leo"Amesema Mbowe.
Viongozi wa chama hicho walikuwa wameitisha maandamano na mikutano ya kisiasa Septemba Mosi kupinga walichosema kuwa ni ukandamizaji unaoendelezwa na serikali.
Baada ya mkutano wa kikao cha Kamati Kuu ya chama Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) mwishoni mwa Julai, viongozi walisema: "Yapo Matukio ambayo yamekua yakifanywa na kukandamiza demokrasia na misingi ikipuuzwa na kudharauliwa."
"Si nia ya Chadema kugombana na Serikali bali ni kazi ya Chama Pinzani kuisaidia Serikali iongoze kwa kufuata misingi ya Katiba," chama hicho kilisema.
Licha ya katazo la Serikali juu ya Maandamano hayo yalipewa jina UKUTA kwa maana ya Umoja wa Kupambana na Udikteta Tanzania, CHADEMA haikuogofya na hivyo ikawa ikijiimarisha kwaajili ya Septemba 1, kwa kufanya vikao kila pembe ya Tanzania vikiwamo vya vya ndani ambavyo vilipigwa marufuku na Polisi, kitendo kilichopelekea viongozi wengi wa chama hicho kushikiliwa na Jeshi la Polisi.
Operesheni UKUTA ilikuwa ni muunganiko wa baadhi ya vyama vya upinzani nchini Tanzania.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment