Image
Image

Kinacho mrudisha nyuma Dullayo kimuziki chafahamika.

Msanii wa bongo fleva,Dullayo ambaye amewahi kutamba na vibao vyake kama naumia roho na mida ya kazi amelalamikiwa na majirani kwa kukithiri kwenye tabia ya ulevi jambo ambalo linamfanya ashindwe kufanya vizuri kisanaa kama alivyokuwa mwanzo na ikizingatiwa hivi sasa music ni ushandani na alishakuwa na jina zuri kupitia muziki. Wakiongea kwenye kipengele cha Cheche kinachopatikana kwenye kipindi cha E-Newz cha East Africa TV kinachozungumzia maisha ya mastaa wakiwa mtaani,majirani hao ambao wengi walimsifu Dullayo kwa kutokuwa na maringo kama mastaa wengine walisema tatizo la msanii huyo ni Ulevi hivyo akiacha ama kupunguza ulevi kitamsaidia na atafanya vizuri katika muziki kama wanavyofanya wengine.
Kusema kweli Dullayo ni msanii mzuri,mdogo wetu,tunaishi naye vizuri katika mtaa wetu lakini kitu kimoja Dullayo anatuudhi anakunywa sana pombe na msanii anapokunywa saana pombe badaye anakuja anaharibika” Kutokana na msanii huyo kuwa na jina baadhi ya washkaji wamemshauri kufanya namna ya kuinua vijana wenzake ambao nao wanafanya muziki ili mwisho wa siku wainuke kama wanavyofanya wasanii wengine kuwainua wanamuziki chipukizi katika mitaa yao.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment