Image
Image

LIPUMBA:CUF inaendeshwa Kiimla,Mimi bado ni Mwenyekiti halali wa CUF.

Na.Salum Msangi,Dar es Salaam. 
..............................................................................................
Aliyekuwa Mwenyekiti wa CUF Ibrahim Lipumba amesema kuwa yeye ni Mwenyekiti halali wa CUF kwani tayari amekwisha muandikia barua msajili wa vyama vya Siasa nchini Bw.Francis Mutungi kwa ajili ya kumjulisha kwamba alitengua barua yake ya kujiuzulu uenyekiti wa CUF mwaka jana na pia alisha mueleza Katibu Mkuu wa chama hicho cha CUF Maalim Seif Sharif Hamad kwamba alitaka kuanza kazi rasmi kuanzia June 10 mwaka huu lakini katibu huyo alimueleza kuwa anatafuta ushauri wa kisheria ambapo mpaka hivi leo hajapewa ushauri huo wa Kisheria.
Kauli hiyo ya Profesa Lipumba anaizungumza zikiwa ni sa kadhaa tangu wavuliwe uanachama wa CUF na Baraza Kuu la Chama hicho lililofanya mkutano wake visiwani Zanzibar kwa lengo la kuwajadili wanachama kadhaa wakiwemo vigogo hao.
"Sisi hatukupewa taarifa yeyote, hatujapewa taarifa ya tuhuma na wala taarifa ya hukumu iliyotolewa tumesikia kwenye vyombo vya habari,taarifa hiyo sisi hatuikubali"Amesema Lipumba.  
Katika kuzungumzia kilicho amuliwa na Baraza kuu la CUF Ibrahimu Lipumba amesema kuwa uamuzi huo hauna mashiko kwani kikao hicho hakikuwa na uhalali hata chembe, kwakuwa Naibu Katibu mkuu Bi.Magdalena Sakaya ambaye ndio msaidizi mkuu wa Katibu Mkuu hakuhusishwa kabisa katika kikao hicho kilicho toa maamuzi na hawakuwapo wajumbe wakutosha kutoka Tanzania bara hivyo kikao hicho sio kikao rasmi wala sihalali.
Kuhusu Prof.Lipumba kutokuelewana na Maalim Seif amesema kuwa, Katibu mkuu huyo amekuwa akikiendesha chama hicho cha CUF ndivyo sivyo kwani amekuwa hampi heshima inayostahili Naibu Katibu Mkuu, hamshirikishi katika mambo mbalimbali kutoka bara ambaye kikatika ndiye msaidizi wake mkuu kwani utaratibu huo umekuwa sio mzuri.
"Maalim Seif anambagua Naibu Katibu Mkuu,anafanya maamuzi bila hata kumshirikisha huu sio utaratibu mzuri, huu ni utaratibu wa kiimla"Amesema Lipumba.
Prof.Lipumba ameenda mbali zaidi huku akisema kuwa kwa hivi sasa vyama vyote vya kidemo Krasia havikai hata kidogo nakuanza kupanga kuwafukuza uanachama wanachama wao.
 "Ukiwa unafukuza wanachama unajitangaza wewe kwamba nichama cha KIDIKTETA, chama cha KIIMLA kwahiyo sisi tunahitaji chama cha kuwa sawa kwa wote, chama ambacho kinafuata misingi mizuri ya Demokrasia"Amesema Lipumba.
Mara baada ya Baraza kuu la CUF kumteua Bw.Julius Mtatiro kuwa Mwenyekiti wa chama hicho kwa muda wakati taratibu zingine zikiendelea, Lipumba amesema kuwa ndani ya chama hicho Mtatiro hawezi kupewa nafasi hiyo nyeti.
"Julius Mtatiro sio Mwenyekiti wa Muda, Julius Mtatiro nilimteua mimi kuwa mjumbe wa mkutano Mkuu, hana uanachama wowote yule,na mimi ndio nimemuingiza hata kwenye kamati ya utendaji, kwahiyo Mtatiro hawezi kuwa Mwenyekiti ameshindwa hata kukiondoza kikao cha Mkutano Mkuu na ndio maana vurugu ikatokea"Amesema Lipumba.
Aidha Prof.Lipumba amesema kuwa licha ya kadhia hizo zinazojitokeza ndani ya chama lakini Chama hicho anawahakikishia wanachama wake kuwa kipo imara, waendelee kukienzi na kuwataka wawe na subira kwani Mwenyekiti wao yupo imara na sasa yupo ngangari kinoma, kwani suala linaloelezwa kuwa ametenguliwa uanachama hazina ukweli kwakuwa kikao hicho kilikuwa sihalali cha kumtengua, kwani yeye ameteuliwa na Mkutano Mkuu.
    
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment