Image
Image

Watu 15 wapoteza maisha kufuatia shambulizi la kujitoa mhanga kwenye ukumbi wa harusi Baghdad.

Watu 15 wameripotiwa kupoteza maisha kufuatia shambulizi la kujitoa mhanga lililotekelezwa kwenye ukumbi wa harusi ulioko kusini mwa mji mkuu wa Baghdad nchini Iraq.
Watu wengine 26 pia wameripotiwa kujeruhiwa kwenye shambulizi hilo lililotekelezwa kwa kutumia vilipuzi vya chupa na mabomu.
Vyanzo vya polisi vimetoa maelezo na kuarifu kwamba shambulizi hilo limetekelezwa na wahusika 5.
Mmoja wa washambuliaji hao alijilipua huku wengine 3 wakiangamizwa na vikosi vya usalama kwenye makabiliano. Mshambuliaji mmoja alifanikiwa kutoroka.
Maelezo zaidi yanaarifu kwamba baadhi ya washambuliaji hao walikuwa wamevalia sare za kijeshi ilhali wengine wao walikuwa na mavazi ya kawaida.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment