Image
Image

Magufuli akataa maji ya ‘geresha’ Shinyanga

RAIS John Magufuli ametoa agizo la maji yaliyokuwa yametoka siku moja kabla ya kufika Kata ya Tinde katika Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga yasiwe nguvu ya soda ya kutoka siku hiyo kwa kumuona yeye na baada ya hapo kutoendelea na kuwafanya wananchi kuendelea kuteseka. Hayo aliyasema jana baada ya Diwani wa kata hiyo, Jafari Kanoro kupewa ruhusa ya kusalimia wananchi wake na kumueleza Rais kuwa changamoto kubwa iliyokuwepo ni uhaba wa maji ambapo jana yake yalianza kutoka rasmi baadhi ya maeneo baada ya kazi iliyofanywa usiku na mchana na mafundi.
Ilielezwa mkutanoni hapo kuwa, maji hayo yametoka baada ya miaka mitatu ya mateso ya kukosa maji safi na salama.
Rais Magufuli alisema kilio cha wananchi hao amekisikia, hivyo kama maji hayo yametoka kwa siku hiyo yasiwe nguvu ya soda, bali yawe endelevu kwa siku zote ikiwa bado kuna mradi mkubwa wa maji kutoka Ziwa Victoria utakaopita Tinde na kuelekea mkoani Tabora.
“Mimi ndugu zangu nasema kuwa mradi wa maji tayari tumepewa kiasi cha shilingi milioni 600 na Serikali ya China, hivyo fedha hizo tutazisambaza kwenye mikoa mbalimbali yenye uhitaji wa mradi wa maji ambapo hata hapa Tinde nitawahurumia kuwatengea fungu hilo,” alisema Rais Magufuli.
Aliwaambia wananchi wa eneo la Isaka na Kagongwa kuwa changamoto ya uhaba wa maji ataitatua, hivyo wamuunge mkono na kumuombea ili atimize ahadi zake alizokuwa akiziahidi kipindi cha uchaguzi.
Pia alisema kitendo cha wanawake kuchota maji umbali mrefu kinamsikitisha ikiwa hali hiyo nayo imeonekana kuchangiwa kwa maambukizi ya virusi vya ukimwi (vvu) kwa baadhi yao kufanyiwa vitendo vya ukatili hasa kubakwa wakati wa kutafuta maji.
Mbunge wa Jimbo la Solwa, Ahmed Salum alisema ameshukuru Serikali ya Awamu ya Tano kumpatia mradi wa maji ambao umeanzia Kata ya Tinde ukitarajiwa kunufaisha vijiji 30.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment