Image
Image

Simba kuibana mbavu Polisi Dodoma kwenye uwanja wa Jamhuri.



KLABU ya Simba inatarajia kucheza mechi ya kirafiki na timu ya Polisi Dodoma Jumamosi kwenye Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba, Haji Manara, alisema kuwa mchezo huo unachezwa kutokana na maombi ya Chama cha soka cha mkoa huo (DOREFA) ili kwenda kuinua morali ya soka.
Manara alisema timu hiyo itaondoka kesho kuelekea Dodoma tayari kwa ajili ya mchezo huo.
“Kama mnavyojua michezo ya Ligi Kuu imesimama kutokana na majukumu ya timu ya taifa ambayo ina wachezaji wetu sita, tumeona ni vyema basi kulifanyia kazi ombi la wenzetu wa Dodoma,” alisema Manara.
Alisema mchezo huo utakuwa sehemu ya maandalizi kwa kocha Joseph Omog kuelekea mechi ya Ruvu Shooting itakayofanyika Septemba 7, mwaka huu.
Simba imevuna pointi nne kutokana na mechi mbili za ligi ilizocheza, ikipata ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Ndanda FC na ikitoka suluhu dhidi ya JKT Ruvu ya Pwani.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment