Image
Image

Makubaliano ya Paris kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa imefanyika New York

Sherehe ya ukabidhi wa nyaraka za nchi zinazoidhinisha Makubaliano ya Paris kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa imefanyika New York, makao makuu ya Umoja wa Mataifa.
Akizungumza kwenye sherehe hiyo, katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema, hadi sasa nchi 60 ambazo zinatoa asilimia 47.5 ya hewa zinazoweza kusababisha kuongezeka kwa joto duniani zimekubali kujiunga na makubaliano hayo, na inamaanisha moja kati ya masharti mawili ya kutekelezwa rasmi kwa makubaliano hayo limetimizwa.
Kwa mujibu wa kanuni zinazohusika, ni sharti kuwa zaidi ya nchi 55 zilizosaini Mkataba wa mfumo wa mabadiliko ya hali ya hewa ya Umoja wa Mataifa zikubali kujiunga na makubaliano hayo, ambao utoaji wao wa hewa zinazosababisha kuongezeka kwa joto duniani unachukua zaidi ya asilimia 55, ili makubaliano ya Paris yatekelezwe rasmi ndani ya siku 30 zinazofuata.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment