Image
Image

Pato la taifa limeendelea kukua kwa kasi ya asilimia 7.9

OFISI ya Taifa ya Takwimu (NBS) imebainisha kuwa katika kipindi cha robo ya pili ya mwaka huu, pato la taifa limeendelea kukua kwa kasi ya asilimia 7.9 ikilinganishwa na asilimia 5.8 ya robo ya pili ya mwaka jana. Aidha, imetaja sekta zilizochangia kukua kwa kasi kwa pato hilo kuwa ni kilimo, viwanda,uchukuzi, ujenzi, madini na umeme kupitia gesi asilia.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam kuhusu taarifa hiyo ya uchumi kwa kipindi cha robo ya pili ya mwaka huu, Mkurugenzi Mkuu wa NBS Dk Albina Chuwa, alisema kutokana na kasi ya uchumi inavyokwenda kwa sasa, huenda ifikapo Desemba mwaka huu, kwenye taarifa ya robo ya tatu ya mwaka, pato hilo likaongezeka zaidi.
Alisema kwa mujibu wa takwimu zilizopo pato hilo la taifa limefikia jumla ya thamani ya Sh trilioni 11. 7 ikilinganishwa na Sh trilioni 10.9 katika kipindi kama hicho cha mwaka jana.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment