Image
Image

Wanachama wa OPEC wafanya makubaliano ya kiwango cha uzalishaji wa mafuta kwa siku

Muungano wa mataifa ya uzalishaji wa mafuta OPEC, umefanya makubaliano mapya kuhusu suala la uzalishaji kwa siku.Kulingana na uamuzi uliochukuliwa na OPEC, uzalishaji wa mafuta kwa siku utatekelezwa kwa wastani wa kiwango cha mapipa milioni 32.5.
Hapo awali, kiwango hicho cha uzalishaji wa mafuta kwa siku kilikuwa ni mapipa milioni 33.24.
Hata hivyo, nchi nyingine zilizoko ndani ya muungano huo kama vile Iran, Nigeria na Libya hazitoathirika kwa uamuzi huo.
Mwenyekiti wa OPEC Muhammed bin Salih es-Sade ametoa maelezo na kuarifu kwamba uamuzi huo utatangazwa rasmi kwenye mkutano utakaofanyika Novemba.
Muungano wa OPEC ulioundwa tarehe 14 Septemba 1960 katika mji mkuu wa Baghdad nchini Iraq, unajumuisha wanachama 14.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment