Image
Image

UKUTA wa CHADEMA waota mbawa kwa mara nyingine.

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimeahirisha tena mikutano na maandamano yake nchi nzima iliyokuwa na jina la Ukuta ambapo safari hii hayajatajwa tarehe nyingine, kitu ambacho kinaonekana kwamba yameota mbawa.
Akizungumza na waandishi wa habari 30 Septemba jijini Dar es salaam, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amesema hawataji tarehe nyingine ili kukwepa maandalizi ya Serikali yanayoweza kuwadhuru wanachama wao.
Mh.Mbowe amesema sababu ya kuahirisha Ukuta ni kutokana na kukosa ushirikiano kutoka kwa viongozi wa dini waliowaomba waahirishe ili wakazungumze na viongozi wa Serikali.
Itakumbukwa kwamba mpaka kufikia hivi leo tayari imefikia Mwezi mmoja baada ya Chadema kusitisha Operesheni yake ya Ukuta iliyokuwa na lengo la kupinga inachokiita ukiukwaji wa haki za binadamu na ukandamizaji wa demokrasia nchini.
Ambapo Operesheni hiyo ilipangwa kuzinduli
wa Septemba mosi nchini kwa maandamano na mikutano ya hadhara kama maazimio ya Kamati Kuu ya Chadema, baada ya chama hicho kukumbwa na vikwazo kadhaa kuendesha shughuli zake, ikiwa ni pamoja na kuzuiwa kufanya mikutano ya hadhara.
ikumbukwe kwamba Siku moja kabla ya kufanyika kwa operesheni hiyo ya UKUTA ya Septemba Mosi, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe aliutangazia uma wa watanzania kwamba wanasitisha maandamano hayo kwa mwezi hadi 1 Octoba 2016, ili kutoa fursa kwa viongozi wa dini kuzungumza na na Rais John Magufuli na Serikali yake ili kuona namna itakavyo kuwa.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment