Image
Image

Warioba aitaka serikali kutekeleza sera zilizowekwa na waasisi wa Taifa.

Serikali imetakiwa kuhakikisha kuwa na itikadi thabiti katika kutekeleza sera zilizowekwa na waasisi wa taifa katika kuondoa ujinga, maradhi na umasikini ili kuleta maendeleo haraka kwa wananchi wake
Hayo yamezungumzwa na Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba, katika Mhadhara wa tatu wa Kigoda cha Mwalimu Nyerere ambao ulikuwa unazungumzia elimu ya juu katika maendeleo ya Afrika.
Jaji Warioba amesema kuwa sasa Tanzania imekosa sera madhubiti ya kiitikadi na kutegemea zaidi matukio na watu na kusema endapo kutakuwa na sera itikadi madhubuti itasaidia kulipeka taifa mbele katika maendeleo.
Amesema vijana wengi wanaimba wimbo wa kutaka maendeleo kwa kuimba wimbo wa kufuta ujinga, maradhi na umasikini bila kujua waasisi wa taifa walitumia mbinu gani katika kufanikisha kuleta maendeleo kwa wananchi.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment