Image
Image

TAMWA yampongeza Rais Magufuli na rais wa Zanzibar Dr. Ali Mohamed Shein kwa uteuzi wa viongozi.


Chama cha Wanahabari Wanawake nchini- TAMWA kinampongeza rais John Pombe Magufuli na rais wa Zanzibar Dr. Ali Mohamed Shein kwa uteuzi wa viongozi na hasa wanawake  ambao wameteuliwa kwa kuwa na imani kuwa wataongeza ufanisi wa kazi katika nafasi zao mbalimbali za maamuzi kwa maslahi ya jamii na taifa zima.
Uteuzi huo ambao umefanyika hivi karibuni, Chama cha TAMWA kimepata viongozi ambao ni wanachama wake wanne walioteuliwa na rais Magufuli pamoja na rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambapo TAMWA tunajivunia na kuwaomba wote walioteuliwa wajitume kwa bidii zaidi ili wawe mfano kwa wengine.
Wanachama wa TAMWA walioteuliwa pamoja na nafasi zao ni Mahfoudha Alley Hamid (Ummie) ambaye amekuwa Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi ya shirika la magazeti ya serikali Zanzibar, Maryam Hamdan – Mwenyekiti wa baraza la sanaa na sensa ya filamu na utamaduni Zanzibar, Nasra Mohamed Juma – Naibu Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC), Rahel Mhando – Katibu Tawala Wilaya mpya ya Kigamboni.
Aidha; TAMWA inawapongeza Rais na makamu wake Samia Suluh Hassan kwa kuona umuhimu wa kuongeza wanawake katika nafasi za ngazi za juu za uongozi kwa kuwa mwanamke ana mchango mkubwa katika kutetea maslahi na maendeleo ya nchi.
TAMWA inaamini kuwa, katika kuleta mabadiliko ya kimaendeleo nchini, uteuzi wa wanawake katika nafasi za juu ni fursa itakayowezesha kuondolewa kwa mapungufu yaliyopo kiuongozi ili kuwepo usawa na haki kwa watanzania wote – wanawake na wanaume.
Aidha; TAMWA inaamini kuwa bado wapo wanawake wanawake wengi wenye uwezo ambao mchango wao unahitajika katika kuleta mabadiliko ya kimaendeleo hapa nchini.
Edda Sanga
Mkurugenzi Mtendaji
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment