Image
Image

Waziri mkuu Binali Yıldırım akutana na mwanamfalme wa Saudi Arabia Muhammed bin Nayif bin Abdulaziz es Suud mjini Anakara

Mwanamfalme wa Saudi Arabia Muhammed bin Nayif bin Abdulaziz es Suud alitekeleza ziara yake ya Uturuki na kukutana na waziri mkuu Binali Yıldırım kwenye makao makuu ya Çankaya mjini Ankara.Hafla maalum ya mapokezi iliandaliwa na baadaye Yıldırım na mwanamfalme wakafanya mazungumzo wakati wa mlo wa jioni.
Mawaziri kadhaa pamoja na viongozi wengine wa ngazi za juu serikalini pia walishiriki mazungumzo hayo.
Viongozi hao walijadili suala la ushirikiano katika sekta za uchumi na nishati zitakazonufaisha Uturuki na Saudi Arabia.
Waziri mkuu Yıldırım alitoa shukrani za dhati kwa Saudi Arabia kwa kuonyesha msimamo wake wa kuunga mkono serikali ya Uturuki dhidi ya jaribio la mapinduzi ya Julai 15.
Wakati huo huo, viongozi hao walikumbushiana umuhimu wa kuweka ushirikiano katika suala la mapambano dhidi ya ugaidi.
Yıldırım pia alifahamisha umuhimu wa ziara ya mwanamfalme wa Saudi Arabia katika masuala mengine ya kikanda kama vile mzozo wa Syria na hali ya maendeleo ya mataifa ya Ghuba.
Kwa upande mwengine mwanamfalme pia alibainisha nia ya Saudi Arabia ya kuimarisha uhusiano wake na Uturuki kufuatia mkutano wa rais Erdogan na Mfalme Salman hapo awali.
Viongozi hao walimalizia mazungumzo kwa kujadili suala la ulinzi na usalama wa kanda ili kuhakikisha hali ya amani na utulivu inaimarika.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment