Image
Image

Auawa kwa kupigwa risasi kwa kumchoma kisu askari wa kulinda ubalozi Kenya.

MTU mmoja Mkenya ameuawa kwa kupigwa risasi baada ya kumchoma kisu askari aliyekuwa akilinda ubalozi wa Marekani jijini Nairobi nchini Kenya. Kamanda wa Polisi wa wilaya ya Girigiri katika jijini la Nairobi Vitalis Otieno amesema polisi wamemuua mtu huyo na kwamba, jina lake halitatolewa wakati tukio bado liko wenye uchunguzi.
Amesema lengo la mtu huyo kumshambulia askari bado halijajulikana. Askari alichomwa kisu kichwani.
"Askari alijibu shambulio kujilinda na amefanikiwa kumuua mshambuliaji. Ofisa wangu amelazwa hospitali katika hali imara. Mtu huyo amekufa papo hapo," alisema Otioano.
Taarifa zaidi kuhusu majeraha aliyepata askari huyo hazijafahamika.
Ubalozi wa Marekani umethibitisha kuwa mtu huyo ameuawa nje ya eneo lake na kwamba hakuna mfanyakazi wa ubalozi aliyehusika katika tukio hilo.
Ubalozi wa Marekani uko wilaya ya Girigiri katika jiji la Nairobi ukiwa miongoni mwa balozi kadhaa na ofisi za Umoja wa Mataifa.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment