Image
Image

Simba si ya mchezomchezo yalibonyeza kizenji toto la Yanga.

SIMBA jana iliendelea kuwapa raha mashabiki wake baada ya kuifunga Toto Africans mabao 3-0 katika mechi ya Ligi Kuu Bara iliyochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam. Ushindi huo umeifanya timu hiyo izidi kujichimbia kileleni mwa msimamo wa ligi ikiwa na pointi 29 katika mechi 11 ilizocheza huku Toto ikibaki mkiani ikiwa na pointi zake nane katika mechi 12.
Mara kadhaa Toto huisumbua Simba zinapokutana, msimu uliopita zilitoka sare katika mechi ya kwanza na timu hiyo ya Mwanza kuibuka na ushindi katika mechi ya marudiano.
Muzammil Yassin ndiye aliyeanza kuamsha shangwe za mashabiki wa Simba baada ya kufunga bao la kuongoza katika dakika ya 43 kwa kuunganisha pasi nzuri ya Fredrick Blagnon.
Toto walicheza mchezo wa kuzuia karibu muda wote wa kipindi cha kwanza, hali iliyosababisha kwenda mapumziko wakiwa nyuma kwa bao hilo moja.
Dakika chache baada ya kuanza kipindi cha pili Blagnon alilazimika kutoka baada ya kuumizwa na beki wa Toto na hivyo nafasi yake kuchukuliwa na Laudit Mavugo.
Mavugo raia wa Burundi hakufanya kosa kwani katika dakika ya 52 aliiandikia Simba bao la pili. Alifunga bao hilo baada ya kupokea pasi safi ya Mohamed Ibrahim ‘Mo’na kuunganisha mpira moja kwa moja nyavuni na kumuacha kipa wa Toto Mussa Kirungi asijue la kufanya.
Muzammil aliwanua tena mashabiki wa Simba katika dakika ya 74 alipofunga bao la tatu kwa kuunganisha mpira wa kona uliochongwa na Said Ndemla na mpira kwenda moja kwa moja wavuni.
Katika mechi nyingine ya ligi iliyochezwa jana kwenye uwanja wa Sokoine Mbeya wenyeji Prisons walilazimishwa sare ya bao 1-1 na Mbao. Matokeo hayo yanaifanya Prisons kufikisha pointi 16 na Mbao pointi 13 katika msimamo wa ligi hiyo.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment